Michezo

PICHA: Solskjaer kaamua kwenda kuwaomba radhi mashabiki wa Man United

on

Ndoto ya club ya Man United kumaliza TOP 4 msimu huu inaweza kuyeyuka licha ya kuwa tayari wamebakiwa na michezo minne kabla ya Ligi Kumalizika, Man United kufuatia kipigo chake cha 4-0 leo kutoka Everton ndio kimewadhoofisha na kuanza kuua matumaini ya mashabiki wao kuona kama timu yao inaweza kumaliza TOP 4.

Lengo na nia ya mashabiki wa Man United ni kuona timu yao inarudi TOP 4 msimu huu ili ipate tiketi ya kucheza UEFA Champions League msimu wa 2019/2020, ila kutokana na game kusalia chache huku vita ya Arsenal, Chelsea na Tottenham kuwa kubwa inaongeza hofu kwa mwenendo wa Man United kumaliza TOP 4, ukizingatia katika game zake 5 zilizopita za mashindano yote wamepoteza game zote.

Baada ya kipigo hicho cha 4-0 kutoka kwa Everton kilichowafanya washindwe kuishusha Chelsea nafasi ya tano, kimewafanya Man United waendelee kubakia nafasi ya 6 wakiwa na point 64, kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer  baada ya game kumalizika aliamua kwenda kuwaomba msamaha wa mashabiki wa Man United kwa matokeo mabovu, mashabiki hao inaaminika wamesafiri kutokea jiji la Manchester hadi katika jiji la Liverpool kuisapoti timu yao ambayo imepoteza mchezo kwa idadi kubwa ya mabao.

“Everton walikuwa bora kwa kila kitu kuna vitu vingi tunahitaji kufanya kwa ubora leo ili kupata matokeo, hatujacheza vizuri hivyo ndio ninavyoweza kusema hatustahili kuwa timu ya Man United tunanyoosha mikono yetu juu na kuomba msamaha, hakuna pakujificha ni wazi hatukuwa bora leo”>>> Ole Gunnar Solskjaer

Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23

Soma na hizi

Tupia Comments