Habari za Mastaa

Jay Z aibuka mshindi mbele ya Wanasheria wake waliomshtaki

By

on

Kwa mujibu wa mtandao wa The Blast umeripoti kuwa rapper Jay Z ameshinda kesi iliyokuwa imefunguliwa na timu ya Wanasheria wake wawili Roschier na SEB toka nchini Sweden baada ya kuripoti kuwa hawajalipwa kikamilifu.

Wanasheria hao walifungua shtaka wakidai kuwa hawakulipwa hela waliostahili na kusema kuwa walikua wakimdai Jay Z kiasi cha Dollar 600,000 za Kimarekani sawa na zaidi ya Bilioni 1 za Kitanzania kutokana na msaada waliompa mpaka kufanikiwa kununua mtandao wa TIDAL mwaka 2014.

Kampuni ya Jay Z ( Carters Company) imewafungulia mashtaka Wanasheria hao kwa kosa la kutaka pesa nyingi kuliko kiasi walichostahili, huku Jay Z akitoa malalmiko kuwa hawakufanya kazi nzuri kama ilivyoada kwenye mkataba walioandikishiana.

BRIGITTE: “NAOLEWA, HARUSI YA WATU 100 TU.. WATOTO 6, ZITTO KABWE ALINIPA MILIONI 40”

Soma na hizi

Tupia Comments