Mix

Washindi wa 10 years Couple Challenge ndio hawa

on

Siku ya tarehe 14 mwezi wa pili husherehekewa duniani kote kama Siku ya wapendanao, kwa kiingereza Valentine’s Day. Hapa nchini pia siku hiyo inasherehekewa kwa watu kuwanunulia zawadi, kuwatumia jumbe wawapendao ama kwenda maeneo ya kupumzika na migahawa ya chakula.

Kwa upande wa StarTimes wao waliandaa changamoto kupitia mitandao yao ya kijamii changamoto iliyoahamika kama #StarTimes10yearsCoupleChallenge ambapo wateja wao walitakiwa kuweka picha kwenye akaunti zao wakionyesha walikuwa wapi miaka 10 iliyopita na sasa wakiwa na wapenzi wao.

Siku ya tarehe 13 Jumatano kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii waliwatangaza washindi wawili wa changamoto hiyo ambao siku ya tarehe 14 walizawadiwa kupumzika katika hoteli ya kifahari ya Slipway iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam. StarTimes wakigharamia malazi, usafiri pamoja na chakula katika hoteli hiyo iliyoko Ufukweni mwa bahari.

“Tumekuwa kwenye mahusiano kwa miaka 12 sasa mimi na mke wangu, hatujawahi kuwa na Valentine nzuri na ya kipekee kama ya mwaka huu. Kwa kweli tunawashukuru sana StarTimes kwa kutujali wao katika siku muhimu kama hii, tumefurahi sana” Jumanne James Mdoe, mmoja wa washindi, Mbali na zawadi ya mapumziko katika hoteli hiyo StarTimes wametoa zawadi kwa washindi wengine 10.

Imeshinda Simba SC tabu kaipata JB wakati wa kutoka

Soma na hizi

Tupia Comments