Michezo

Arsenal wana kazi ngumu leo, majirani zao Chelsea washindwe wao tu Europa League

on

Arsenal wana kazi kubwa mikononi mwao kama wanataka kuendelea kuuota ubingwa wa Europa mwaka huu, Arsenal walipoteza mchezo kwa mabao 3-1 dhidi ya club ya Rennes inayoaminika kuwa ya kawaida kutoka Ligi ya Ufaransa kwenye mechi ya kwanza ya mzunguko wa 16 bora wiki iliyopita na kwa sasa sasa wanahitaji walau magoli mawili bila majibu ili kufuzu Robo fainali.

Vijana wa Unai Emery walipata ushindi muhimu dhidi ya Manchester United Jumapili na morali yao imeongezeka maradufu, hata hivyo Arsenal watakuwa bila beki wao Sokratis ambaye alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo uliopita.

Kocha huyo anatarajia kumuanzisha mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon Pierre Emerick Aubameyang ambaye alifunga kwa mkwaju wa penati dhidi ya Manchester United kwani anahitaji magoli zaidi ya kitu chochote ili aweze kufuzu.

Kwingineko Chelsea wako katika hali nzuri ukilinganisha na jirani zao wa jiji la London, wao walifunga mabao 3-0 dhidi ya Dynamo Kyiv kwenye mchezo wa kwanza lakini walipoteza point mbili siku ya Jumapili walipokutana na Wolves kwenye Ligi, matokeo ambayo yaliwafanya wasirejee katika nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi.

Kocha Maurizio Sarri anasema, “Ni kombe (Europa) la muhimu sana kwetu. Na kuna nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa kwa bingwa kwa hiyo lengo letu na ni muhimu kwetu kushinda” Napoli ni timu nyingine iliyofanya vizuri wiki iliyopita baada ya kushinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Red Bull Salzburg, huku timu nyingine kutoka Serie A, Inter Milan ilitoka sare na Frankfurt walipokutana wiki iliyopita, game zitaoneshwa ST World Football.

Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke 

Soma na hizi

Tupia Comments