Premier Bet SwahiliFlix Ad Halotel Ad

AyoTV

Msimamo wa Beno Kakolanya Yanga ndio huu, katuma tena barua

on

Zaidi ya miezi miwili sasa toka kocha mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera atangaze kuwa golikipa wake namba moja Beno Kakolanya atafute timu nyingine kwani hana nafasi tena Yanga, hiyo inatokana na golikipa huyo kugoma kwa siku kadhaa kuichezea timu yao akiwa anashinikiza alipwe madeni yake ya pesa za usajili.
Ilielezwa kuwa Kakolanya alikuwa anadai Yanga Tsh Milioni 15 za usajili lakini baada ya mdau wa Yanga kumpa kiasi cha pesa cha Tsh Milioni 2 alitaka kurudo aendelee kuichezea timu hiyo lakini kocha wake Mwinyi Zahera akamkataa na kusema hamuhitaji tena mchezaji huyo kutokana na kugoma.
Leo kaimu mwenyekiti wa Yanga Samwel Lukumay ametangaza rasmi kuwa wanasheria wa Beno Kakolanya wametuma barua nyingine na kueleza kuwa wanataka kuvunja mkataba licha ya Yanga kumlipa stahiki zake, Samwel Lukumay amesema Beno Kalonya ametuma barua nyingine akisitiza kuvunja mkataba na Yanga, hivyo wanasubiri wanasheria wao halafu watamjibu hawana neno na mchezaji ambaye hataki kuichezea club yao.

Ukimuuliza Ajib wa Yanga ishu ya Beno Kakolanya atakujibu hivi

Soma na hizi

Tupia Comments