Pamoja na kuwa mshambuliaji wa Cardiff City aliyepoteza maisha katika ajali ya ndege ndogo Emiliano Sala akiwa ameshazikwa, uchunguzi bado unaendelea ili kubaini chanzo cha ajali hiyo lakini na hitiliafu iliyopolekea ajali ya ndege ndogo iliyokuwa imembeba marehemu Emiliano Sala na rubani wake David Ibbotson kutoka Nantes kuelekea Cardiff.
Sala amezikwa baada ya kutafutwa kwa zaidi ya siku 10 baada ya ndege yao kupotea January 21 lakini mwili wake ulipatikana katika mabaki ya ndege hiyo chini ya bahari, leo zimetoka taarifa kuwa ndege aliyokuwa anasafiria Emiliano Sala na rubani wake haikuwa imesajiliwa kubeba abiria.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Emiliano Sala alisajiliwa na Cardiff City siku tatu kabla ya kifo chake kwa dau la pound milioni 15 akitokea Nantes FC ya Ufaransa, Sala alipata ajali akiwa anarejea Cardiff City January 21 2019 akitokea Nantes kuwaaga wachezaji wenzake.
Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake