Premier Bet SwahiliFlix Ad Halotel Ad

AyoTV

VIDEO: Katibu Mkuu wa TFF aungana na familia ya shabiki aliyefia uwanja wa Taifa

on

Shirikisho la soka Tanzania TFF limeonesha kwa vitendo kuguswa kwa kifo cha mwanafamilia wa michezo mzee Christopher Rupia aliyefariki ndani ya uwanja wa Taifa Dar es Salaam Jumapili ya September 8 2019 akiwa anatazama mechi ya Tanzania na Burundi.

TFF kupitia kwa katibu mkuu wake Wilfred Kidao wameshiriki mazishi ya mwanamichezo huyo, ambaye alipoteza maisha akiwa sehemu ya watanzania waliokuwa wanapambana kwa kushangilia ili timu yao ipate ushindi katika mchezo huo wa kuwania kufuzu kucheza makundi ya kupambania nafasi za kucheza fainali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.

Kidao ameungana na watanzania na watu mbalimbali ikiwemo familia ya marehemu katika maombolezo ya msiba huo, hii sio mara ya kwanza kwa shabiki wa soka kufia uwanjani imewahi kutokea mara kadhaa katika mataifa mbalimbali duniani.

EXCLUSIVE: SAMATTA KAFUNGUKA DILI LAKE KWENDA ENGLAND, VIPI CHAMPIONS LEAGUE

Soma na hizi

Tupia Comments