Shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA leo limetangaza viwango vipya vya soka vya ubora wa FIFA, timu ya taifa ya Tanzania iliyo chini ya kaimu kocha mkuu Etienne Ndairagije imeendelea kuwa na mafanikio kwa kufanikiwa kupanda.
Tanzania leo imefanikiwa kupanda katika viwango hivyo vya ubora kutoka nafasi ya 137 hadi nafasi ya 135 Duniani, viwango hivyo hubadilika kutokana na ratiba ya kalenda ya FIFA ambapo matokeo yake ndio huwa yanaleta point za kupanda.
Mara nyingi Tanzania imekuwa ni kawaida kupanda na kushuka lakini sasa hivi imeanza kuleta matumaini, hata hivyo kwa ujumla Ubelgiji anaongoza katika viwango hivyo, wakifuatiwa na Ufaransa wakati Brazik wakishika nafasi ya tatu.
VIDEO: Moja kati ya magoli ya marehemu Jeba, hili liliwaumiza wana-Simba 2016