Habari za Mastaa

RC Makonda “Angefariki mitandao yote ingechafuka RIP Ommy”

By

on

Jina la mwimbaji Ommy Dimpoz limechukua headlines baada kukanyaga ardhi ya Bongo February 5,2019 kutokea nchini Ujerumani alipokwenda kwa ajili ya kufanyiwa operesheni ya pili baada ya kukutwa na tatizo tena katika mfumo wake wa chakula.

Ommy Dimpoz alichukua nafasi ya kumshukuru Mungu kwa njia ya wimbo unaoitwa ‘Ni wewe’ aliouchia rasmi February 5,2019 ikiwa lengo ni kusukuru kwa kila kitu alichopitia mpaka kufikia kukata tamaa lakini kwa sasa afya yake inaimarika.

Kupitia ukurasa wa instagram wa RC Paul Makonda amefunguka kuhusu watu kuonyesha upendo pale alipokuwa mgonjwa na kumuandikia maneno ya kumfariji lakini kwa sasa ameachia ngoma mpya ila upendo ule hauonekani tena.

“Ukitaka kujua watu walivyo wa Ajabu tazama leo, Ommy dimpo alikuwa mgonjwa sana na ikafika hatua ya watu kutangaza Amekufa. Leo amerejea tena akiwa na wimbo wa kumshukuru Mungu wamekaa kimya Kama vile siyo wao waliokuwa wana post kumwombea apone”

“Angefariki tungeona mitandao yote imechafuka RIP Ommy oooh umeenda bado tunakuhitaji. Unafiki huu sijuwi utaisha lini, tunapenda kutangaza msiba kuliko uponyaji”

EXCLUSIVE: MREMBO POSHY ALIYEKAMATIA FURSA YA UMBO LAKE NA KUUZA VIGODORO  

Soma na hizi

Tupia Comments