Habari za Mastaa

Kifungo cha miaka 30 jela cha mnyemelea R. Kelly

on

Baada ya mtandao wa ‘The Blast’ kuripoti kuhusu mwimbaji R. Kelly kufunguliwa mashtaka mengine 11 ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya wasichana wadogo sasa imeelezwa kuwa nguli huyo ameendelea kukana mashtaka hayo ambayo yalifunguliwa siku ya Alhamis May 30,2019.

Inaelezwa kuwa June 6,2016 R. Kelly alipandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Cook mjini Chicago ili kujibu mashtaka yote 11 ambapo makosa manne yalitajwa kupewa daraja X na kuwekwa kwenye kipengele cha makosa ya jinai na huenda nguli huyo akahukumiwa miaka 30 jela endapo akikutwa na hatia.

Mwanzoni mwa mwaka huu mwimbaji huyo alikabiliwa na mashtaka 10 ya unyanyasaji wa kingono hata hivyo alikana kuhusika na vitendo hivyo na aliaachiwa huru kwa dhamana yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 200 za Kitanzania.

VIDEO: DOGO JANJA KWENYE JUKWAA LA NANDY FESTIVAL SUMBAWANGA

Soma na hizi

Tupia Comments