Michezo

Man United imeishindwa Arsenal baada ya kutopoteza katika game 13

on

Baada ya kuwa na mwanzo mzuri akiwa na Man United kama kocha wa muda Ole Gunnar Solskjaer leo ameanza kukutana na kigingi katika Ligi Kuu ya England baada ya kukaribishwa na vijana wa Unai Emry katika uwanja wa Emirates na kucheza mchezo wao wa 191 dhidi ya Arsenal.

Wakiwa Emirates Man United wamejikuta wakikubali kipigo cha magoli 2-0, magoli ya Arsenal yakitupiwa wavunia na Granit Xhaka dakika ya 12 na Pierre Emerick Aubameyang dakika ya 67 kupitia mkwaju wa penati na kujihakikishia kuwa point tatu zinasalia Emirates na kuvunja rekodi ya Man United chini ya Ole Gunnar Solskjaer.

Kipigo hicho kiwakuwa cha kwanza kwa Man United katika EPL toka wawe chini ya kocha wao Ole Gunnar Solskjaer ambaye amewaongoza katika michezo 13 hadi sasa wakitoka sare michezo miwili, haya hivyo Arsenal pia inakuwa timu ya kwanza msimu huu kucheza na Man United nyumbani na kufanikiwa kumaliza game kwa clean Sheet(bila kuruhusu goli katika mchezo).

 

Matokeo ya EPL March 10 2019.

Msimamo wa EPL ulivyo kwa sasa.

Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake

Soma na hizi

Tupia Comments