Michezo

Dalili nyingine ya Zlatan Ibrahimovic kuelekea kujiunga na Man United

on

Usiku wa June 9 taarifa za staa wa zamani wa klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Zlatan Ibrahimovich kuhusishwa kujiunga na klabu ya Man United zimechukua sura mpya, Zlatan anaripotiwa kukamilisha hatua ya nne ya kujiunga na klabu ya Manchester United.

Dalili inayotajwa kuwa staa huyo yupo mbioni au katika hatua za mwisho kujiunga na klabu ya Man United zinazidi kudhihirika, baada ya kuripotiwa tayari ametafutiwa nyumba ya kuishi katika jiji la Manchester ambapo ndio makao makuu au mji inapotoka klabu ya Man United.

bgv

Kwa mujibu wa nyaraka iliyopostiwa katika websites ya Proto Group Ltd ambao ni mawakala wa nyumba inaashiria kuwa mipango ya Zlatan kutangazwa kujiunga na Man United ipo tayari kutokana na mji alipotafutiwa nyumba ya kuishi, kwani kabla ya hapo alikuwa akiishi Paris Ufaransa.

ALL GOALS: TAIFA STARS VS MISRI JUNE 4 2016, FULL TIME 0-2

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments