Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa jinai ICC imemhukumu kifungo cha miaka 25 Kiongozi wa zamani wa Waasi wa Lord’s Resistance Army, LRA Dominic Ongwen.
Dominic Ongwen, anayefahamika kama White Ant, alipatikana na zaidi ya makosa 60 ikiwa ni pamoja na uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita.
Waendesha mashtaka wanasema kuwa, Ongwen amepewa adhabu ndogo kwasababu alikuwa ametekwa na LRA akiwa mtoto mdogo.
Kundi hilo la waasi liliundwa zaidi ya miaka 30 iliyopita ikiendesha shughuli zake nchini Uganda na mataifa jirani.