Duniani

Sio kila parking iko salama, unaweza kukuta gari yako imegeuka barafu kama hii !! (Picha & Video)

on

Shabiki mmoja wa mpira wa miguu aliingia zake uwanjani Hamburg, New York Marekani…. akaingia zake ndani ili kujienjoy na watu wake game ya American Football !! Kutoka nje kakuta mambo ndivyo sivyo.

Sehemu ambapo gari hiyo imepaki ni jirani kabisa na ziwa Erie, mwenye gari ni Justin Yelen ambaye alikuwa na washkaji zake ambao baada ya kuangalia game ya mpira waliendelea zao kujienjoy mida isogee sogee.

WINTER II

Baada ya Justin na washkaji zake kulewa waliona haitokuwa poa wakiondoka wanaendesha gari na wamelewa… wakaacha gari parking, baadae jamaa kurudi ndio hivyo akakutana na gari imefunikwa na barafu… baridi kali na upepo kutoka kwenye ziwa hilo vimechangia gari hiyo kufunikwa na barafu.

Video ya gari yenyewe hii hapa… kama joto la Dar es Salaam linatesa, basi ujue mtu wangu hata baridi lina balaa lake kama hivi !!

https://www.youtube.com/watch?v=nSJ2qWYyN_s

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments