Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na wizara ya afya ya Zambia, zinaonesha kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na mlipuko wa kipindupindu nchini humo imeongezeka hadi 222, na watu 5,462 wameambukizwa tangu kuzuka kwa mlipuko huo Oktoba mwaka jana.
Takwimu ziliyotolewa jumapili na wizara hiyo zinaonyesha kuwa watu 27 wamekufa na wengine 567 wameambukizwa katika saa 24 zilizopita.
Wizara hiyo pia imesema watu 340 wamepona na kuondoka hospitali katika kipindi hicho, na kwa ujumla idadi ya watu waliopona imefikia 4,172, wakati idadi ya watu walioko hospitalini inafikia 1,059.