Mamlaka ya eneo la Gaza, Jumatatu, ilisema idadi ya vifo vya Wapalestina kutokana na mashambulizi mabaya ya Israel kwenye eneo hilo sasa inazidi 15,000, pamoja na maelfu ya wengine ambao bado hawajulikani walipo chini ya vifusi, Shirika la Anadolu linaripoti.
Katika taarifa yake, Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Serikali yenye makao yake makuu Gaza ilisema idadi ya waliofariki ni pamoja na watoto 6,150 na wanawake 4,000, pamoja na idadi isiyojulikana ya maiti zilizotawanyika mitaani.
Imeongeza kuwa pia kuna takriban watu 7,000 waliopotea chini ya vifusi, wakiwemo watoto 4,700 na wanawake.
Taarifa hiyo ilibainisha kuwa, miongoni mwa Wapalestina waliokufa, ni wahudumu wa afya 207, wanachama 26 wa timu za uokoaji za ulinzi wa raia na waandishi wa habari 70.
Zaidi ya Wapalestina wengine 36,000 pia walijeruhiwa, asilimia 75 kati yao wakiwa watoto na wanawake, ofisi hiyo iliongeza.
Kuhusu majengo ya makazi, ilisema karibu nyumba 50,000 ziliharibiwa kabisa pamoja na karibu nyumba 240,000 zilizoharibiwa vibaya.
Jumla ya misikiti 88 iliharibiwa kabisa na mingine 174 kuharibiwa kwa sehemu na mashambulizi ya Israel katika eneo la Gaza, pamoja na makanisa matatu yaliyolengwa na jeshi la Israel.