Idadi ya wanyama pori wanaogongwa katika Barabara ya Babati- Arusha imetajwa kuongezeka nakufikia jumla ya wanyama 380 kwa mwaka ikiwa ni sawa na mnyama mmoja kugongwa kwa siku.Hayo yamesemwa wakati wa kikao Cha Wadau wa uhifadhi wa wanyamapori mkoa wa Manyara ambapo jambo hilo linatajwa kuadhiri shughuli za kitalii ikiwa ni pamoja kupunguza mapato kwa Serikali kupitia sekta ya utalii huku afisa wanayamapori mkoa wa Manyara Felix Mwasenga amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau wa uhifadhi wa wanyamapori kuhakikisha Tanrods inaweka alama katika maeneo yanayotajwa ili kutatua changamoto hiyo.
Afisa Mhifadhi mwandamizi Aliningo Swai kutoka TAWA amesema Changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu(Simba na Tembo) inatajwa kuongezeka katika Makazi ya watu kwa baadhi ya maeneo mkoa wa Manyara huku ambapo kwa kushirikiana na taasisi nyingine za uhifadhi wameendelea kutoa elimu kwa wananchi wanoishi jirani na maeneo ya hifadhi ikiwemo kuwapatia vitendea kazi kwaajili ya kukabiliana na changamoto hiyo hasa katika wilaya ya Babati.
Kwa upande wake afisa Mahusiano kutoka Chem chem Association Charles Silvesta amesema sensa hiyo hufanyika Kila baada ya miaka Mitano huku lengo likiwa ni kubaini idadi ya wanyama ambao wapo kwenye eneo la Ikolojia la hifadhi ya Tiafa ya Tarangire na Manyara huku akisema mkakati wao ni kuendelea kujenga Maboma ya kisasa katika vijiji vyenye changamoto hiyo ili kupunguza wimbi la wanyama wakali kuvamia mifugo.