Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Post ya Nay wa Mitego kuhusu Wema Sepetu na Milioni 500 za Idris

on

Nay wa Mitego ni kati ya Mastaa wa Tanzania ambao karibia kila wanachokifanya kwenye maisha yao hugeuka kuwa Headlines kubwa kutokana na style ya vitu wanavyofanya. Leo October 27, 2016 kupitia Instagram Rapa Nay wa Mitego a.k.a True Boy amepost video mbili akiwazungumzia Wema Sepetu na Idris Sultan.

Kwa mujibu wa Video hizo Nay anasikika akihoji kilichomaliza pesa za mshindi huyo wa shindano la Big Brother Afrika msimu wa 2014 na kuondoka na mkwanja mrefu sana kiasi cha shilingi Milioni 500.

Baada ya ushindi wake Idris aliingia kwenye headlines za kudate na mastaa wengine akiwemo mshiriki mwenzake wa shindano la BBA Samantha ambaye waliachana na akaanza kudate na Wema Sepetu ambaye naye ziko stori kwamba wawili hao hawako pamoja japo hakuna aliyethibitisha wala kukanusha mpaka sasa.

Sasa Nay wa Mitego anauliza je zile Milioni 500 za Idris ni mwanamke gani amezimaliza kati ya Wema Sepetu au Samantha.

Nimekuwekea hapa Video ya Nay wa Mitego akihoji pesa za Idris zimeishaje.

ULIMISS ALICHOKISEMA AY KUHUSU KUACHA KUWASIMAMIA OMMY DIMPOZ NA STEREO? ITAZAME HAPA

 

Soma na hizi

Tupia Comments