fB insta twitter

Alichokiandika Idriss Sultan kuhusu Bongo movie

on

Staa wa vichekesho Bongo Idriss Sultan ameonesha hisia zake juu ya issue ya Bongo Movie ambayo ina-make headlines kwa siku za hivi karibuni baada ya waigizaji wa tasnia hiyo kuandamana wakitaka kufungiwa kwa filamu za nje ya nchi.

Kupitia account yake ya Instagram Idriss Sultan ameweka ujumbe mfupi kuhusu kuporomoka kwa industry ya filamu Tanzania akisema atahakikisha anafanya kazi hizo kwa bidii kwa lengo la kukuza soko la movie nchini akidai kuwa yeye bado mdogo sana kwenye tasnia hiyo, hivyo hawezi kulizungumzia na kuwaomba mashabiki waendelee kununua movie ya KIUMENI ambayo imeingia sokoni.

>>>”Mi mdogo sana kulizungumzia suala la bongo movie ntaulizwa najua nini maskini ila kwa juhudi zangu ntahakikisha napiga kazi nzito hata nipewe scene ya kuigiza mama ntilie ntahakikisha mnatamani kununua chakula kibandani kwangu.

“I promised myself juu chini I will get to hollywood for me, for my country na kwa yule anayejiangalia akitamani nifanye vizuri sana awe inspired. Bless all who are fighting kuhakikisha watanzania wanapata kazi nzuri wanazostahili. Kujitoa muhimu wengine tunakomaa mpaka kieleweke. Kiumeni movie sasa ipo madukani kainunue dvd yako hautojuta kabisa. Nilikua jambazi na haki ya Mungu nataka kuwahakikishia sikuvua kiatu mlangoni.” – Idriss Sultan.

VIDEO: “Sinema zetu zina mapungufu mengi lakini hiyo sio sababu za kuacha kudai haki zetu” – JB

 

Soma na hizi

Tupia Comments