Zipo mila nyingi duniani lakini moja sapo ya kabila hili nchini ethiopia imewaacha wengi midiomo wazi ambapo wanaume wanakutana na njia moja ama nyingine ya kutafuta mke katika sherehe zao binafsi ambapo hutumia fimbo kama njia au alama ya mpambano mkali wakuonesha ujasiri wa kuwa tayari kupata mwanamke mrembo.
Sherehe hiyo huitwa ya Donga imejaa nderemo, kuimba, kucheza na kumwaga damu huku mshindi akiwa mume anayetafutwa na mmoja wa wasichana ambao hawajaolewa wakitazama.
Donga, ni sherehe ya kabila la Surma na Mursi, ambapo wanaume hupigana wao kwa wao ili kuonyesha ujasiri wao kwa wanawake na watu wengine.
Wakati wa sherehe hii wanawake wanacheza na kuimba wakionyesha urembo wao, sherehe hudumu siku nzima na wale ambao wameonyesha ujasiri zaidi wataweza kuchagua msichana mzuri wa kijiji.
tazama zaidi..