Serikali imesema upelekwaji wa nishati ya umeme vijijini imefikia 89% ya Vijiji 10987 kati ya Vijiji 12318 vilivyopo nchini huku Vijiji vilivyosalia vikiwa ni 13031ambapo Serikali kupitia Wakala wa Usambazaji Umeme Vijijini Wamekuwa wakipambana kuhakikisha Vijiji vyote vinafikiwa na Huduma ya Nishati ambayo imekuwa ni kichocheo cha Maendeleo kwa Watanzania na Taifa Kwa Ujumla.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) , Hassan Saidi wakati alipokuwa akizungumza na Wandishi wa Habari katika Viwanja vya Maonesho Mjini Geita ambapo amesema mpaka sasa wakandarasi wako kazini na kusema Matarajio yao ifikapo June Mwakani Vijiji vyote viwe vimefikiwa na Umeme.
“Kwa hali ya upatikanaji wa umeme kwa sasa hivi Tanzania ina Vijiji Elfu 12318 na mpaka hivi tunavyo ongea mpaka taarifa ya wiki ya Mwisho ya Mwezi wa nane Vijiji elfu 10987 ambavyo kariba aslimia 89 ya vijiji vyote 12318 vimeshafikiwa na huduma ya Umeme, ” Mkurugenzi Mkuu REA.
Said amesma endapo watakamilisha zoezi la kupeleka umeme kila kijiji watahamia kwenye vitongoji vyote ambapo kwa Tanzania Bara vipo Elfu 64760 ambapo amesema katika hilo karibu Vitongoji Elfu 28586 vimeshafikiwa na Umeme na sasa kuna Vitongoji 36 bado havijafikiwa na Umeme na ndivyo viko kwenye Mchakato huo.
Said amesema Tanzania Itakuwa Nchi pekee kuingia katika historia kwa nchi chache za Afrika ambazo zimeweza kufanikisha kupanua miundombinu ya umeme kwenye Maeneo yote .