Habari za Mastaa

Hii ni kwa wale watu wangu wa Hip-Hop… Iggy Azalea kurudi na album mpya!

on

Msanii kutoka kwenye lebo ya T.I, Hustle Gang, Iggy Azalea amerudi tena kuziteka headlines kwenye kurasa za burudani… staa huyo mwenye asili ya Australia ametangaza kupitia page yake ya Twitter kuwa anarudi kwenye chati na album mpya alioipa jina ‘Digital Distortion’.

Kwenye page yake ya Twitter, Iggy Azalea aliwaambia mashabiki kuwa; “Digital Distortion sio jina la wimbo, ni jina la Album yangu”, tweet iliyokuwa inajibu swali la mmoja ya followers wake kwenye mtandao huo.

Iggy Iggz

Digital Distortion itakuwa album ya pili ya Iggy Azalea, Album yake ya kwanza The New Classic iliotoka mwaka jana na ilibeba nyimbo kama ‘Fancy’, ‘Black Widow’ nyimbo ambazo kwa mwaka 2014 zilibahatika kuchaguliwa kuwania tuzo za Grammy.

Iggy Iggz2

Kwenye Album hii mpya Iggy amefanya ngoma na baadhi wasanii ikiwemo Tinashe

iggy iggz3

Mipango yake kwa sasa ni kuachia single ya utangulizi iliyopewa jina ‘Zillion’ kabla ya kuachia single yake ya kwanza kutoka kwenye album yake mpya. Management ya Iggy Azalea imesema kuwa licha ye yeye kutoa single hizo mbili, Album yake itakuwa sokoni rasmi mwanzoni wa mwaka 2016.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM, TWITTER, FB, YOUTUBE

 

Soma na hizi

Tupia Comments