Michezo

Ighalo azuiwa kuungana na wachezaji wenzake wa Man United

on

Baada ya kumuacha kwenye kambi ya muda mfupi nchini Hispania, imeripotiwa Man United pia imemtaka mchezaji wao Jude Odion Ighalo kufanya mazoezi pekeake na sio na wenzake katika uwanja wa mazoezi wa Carrington.

Ighalo amejiunga na Man United akitokea club ya Shanghai Greenland Shenhua ya China kwa mkopo hadi mwisho wa msimu, hivyo kwakuwa ametokea China ambako kuna hofu ya mlipuko wa virusi vya Corona hajaruhusiwa kujumuika na wenzake.

Sio kwamba Ighalo amegundulika kuwa na virusi hivyo ila amewekwa pembeni kwa tahadhari tu na sio vinginevyo, pamoja nakuwa Ighalo hajatoke Wuhan China ambapo ni chimbuko hasa la virusi hivyo.

Ighalo kwa sasa anafanya mazoezi binafsi jijini Manchester katika kituo cha mchezo wa GB Taekwondo akisimamiwa na na Wayne Richardson hadi Alhamisi hii ndio itakuwa mazoezi yake ya mwisho, hadi sasa inadaiwa watu 1100 wameambukizwa virus vya Corona ambavyo vimeanza kuenea duniani kote.

Soma na hizi

Tupia Comments