Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camilius Wambura ameingilia kati sakata la askari polisi wa wilayani Siha mkoani Kilimanjaro, Koplo Wilfred Kavishe aliyejeruhiwa kwa kukatwa panga kichwani na mtuhumiwa wa mauaii.
IJP Wambura amemtuma Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Ramadhan Kingai, kuongoza timu ya wataalamu kwenda kuchunguza tukio hilo.
Koplo Kavishe alijeruhiwa kwa kitu chenye cha kali na kushonwa nyuzi 12 kichwani, alipokutana na mkasa huo usiku wa Septemba 27, mwaka huu, wakati wa purukushani za kumkamata Pancras Shirima, mkazi wa Kijiji cha Naibili.
Taarifa iliyotolewa Oktoba 2, mwaka huu na Msemaji wa Jeshi la Polisi chini, David Misime, inabainisha kuwa DCI Kingai atafanya uchunguzi wa kilichotokea na kuwahoji waliokuwapo eneo la tukio.