Habari za Mastaa

Hatimae R. Kelly azungumzia sakata lake la unyanyasaji wa kingono (+video)

on

Mwimbaji nguli wa miondoko ya RnB R. Kelly ameamua kufunguka kwa mara ya kwanza baada ya tuhuma zinazomuandama juu ya unyanyasaji wa kingono kwa wanawake 10 waliokuwa chini ya umri wa miaka 18 hadi kumpelekea kujislaimisha mikononi mwa polisi mwezi February 22,2019.

R.Kelly amekanusha tuhuma hizo na kusema kuwa hazina ukweli wowote na watu wanajaribu kuleta vitu vilivyopita na kuvihusisha na hali ya sasa. Nguli huyo ameyasema hayo kupitia mahojiano aliyoyafanya na Gayle King wa CBS ‘This Morning’

“Nilikuwa nina kesi mbili na nimezishinda, watu wanajaribu kuleta vitu vya zamani na kuvihusisha na vya sasa vyote vinavyosema havina ukweli wowote, tumia akili yako hata kama unanipenda au unanichukia siwezi kuwafanyia hivyo wasichana nitakuwa mpumbavu, sikufanya hivyo vitu, huyu sio mimi, nitapigania haki zangu” >>>R. Kelly

PERFECT CRISPIN: “BILA RUGE NISINGEKUWA HAPA, ALIPENDA TUPIGANE”

Soma na hizi

Tupia Comments