AyoTV

Vitu Said Meck Sadiki atavimiss baada ya JPM kulikubali ombi lake

on

Miongoni mwa taarifa zilizotoka kwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu May 16, 2017 ni pamoja na JPM kukubali ombi la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki kuacha kazi katika nafasi hiyo.

Ayo TV na millardayo.com zimempata Said Meck Sadiki na kuzungumza naye ambapo amesema moja ya vitu ambavyo atavikumbuka wakati wa utumishi wake ni pamoja na mahusiano yake na waandishi wa habari kwa sababu wamekuwa mstari wa mbele wakishirikana naye katika kutangaza mafanikio ambayo wananchi huyafurahia.

Aidha, Said Meck Sadiki amebainisha changamoto kubwa ambayo alikabiliana nayo ni pamoja na wakati anahitaji jambo lifanyike, lakini likashindikana hasa katika utekelezwaji wa Ilani ya Uchaguzi

Bonyeza Play hapa chini kusikiliza Full..

Hatua zilizotangazwa na TRA kufuatia agizo la JPM 

Soma na hizi

Tupia Comments