Habari za Mastaa

VIDEO: Alicia Keys apanda stejini na mwanae

on

Kwenye tuzo za iHeartRadio zilizofanyika March 14,2019 nchini Marekani Mwimbaji Alicia Keys alimualika mwanae wa kiume Egypt kwenye jukwaa kwa lengo la kutumbuiza nae, Alicia Keys alianza kuburudisha watu wimbo wa ‘Raise a Man’ na baadae alimualika Egypt kwa ajili ya kupiga kinanda pamoja.

Alicia Keys ameonekana kufurahishwa na kile ambacho mwanae alikifanya mbele ya watu ikiwa sio mara ya kwanza kwa mwanae kufanya kitu kama hicho, kupitia kwenye ukurasa wa instagram wa Alicia Keys amemsifu mwanae na kumuita hodari huku akimshukuru na kujivunia nae.

” Wakati wa mama pamoja na naoto ambayo naiota, wow, Egypt umenishangaza wewe ni hodari na mzuri na unanifanya nijivunie, hisia niliyohisi wakati nikiwa karibu na wewe nilipokua naimba huu wimbo ulinifanya nisisimke, ulitisha mwanangu safari yako ndio inaanza na nimebarikiwa kukuza kijana kama wewe” >>>Alicia Keys

VIDEO: PIERE KAPATA SHAVU LA UBALOZI WA HOTEL KAFUNGUKA, SAA YA GHARAMA KAPEWA NA WEMA

 

Soma na hizi

Tupia Comments