Michezo

Ryan Giggs amejibu dongo la Zlatan Ibrahimovic

on

Ni siku moja imepita tokea staa wa kimataifa wa Sweden anayeichezea club ya LA Galaxy ya Marekani Zlatan Ibrahimovic awakosoe wachambuzi wa soka ambao pia ni wachezaji wa zamani wa Man United Paul Scholes, Ryan Giggs na Gary Neville kwa vitendo vyao vya kupenda kuwakosoa sana wachezaji wa sasa wa Man United.

Giggs na Zlatan

“Hawachezi tena pale (Man United)n wapo kwenye TV na wanalalamika muda wote kwa sababu hawapo tena katika timu, kama unataka kwenda kufanya kazi katika club nenda katafute hiyo kazi, Pogba alikuwa Man United wakati anachipukia halafu alihama na baadae akarudi tena katika utawala wa Ferguson hakuwa anapenda hilo ndio maana hawakuwahi kumuhama Ferguson”>>>Zlatan

Kufuatia kauli aliyoitoa Zlatan Ibrahimovic ambaye pia amewahi kucheza club hiyo, Ryan Giggs ameamua kujibu mapigo kwa kutoa kauli kuwa kama Zlatan anaifahamu club ya Man United zaidi yao sawa lakini wao wamekuwa wakiongea vingi kama mashabiki wa kawaida.

Zlatan Ibrahimovic

“Sisi ni mashabiki ndivyo mpira ulivyo kuwa kuna watu watakuwa na mawazo tofauti tofauti lakini ni wazi inawezekana anaijua (Zlatan) club zaidi yetu”>>> Ryan Giggs

Mashabiki wa Simba na Yanga waiongelea Simba VS AS Vita hapo kesho !!

Soma na hizi

Tupia Comments