Michezo

MO Dewji katangaza jukumu jipya la Crescentius Magori

on

Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya SImba SC Mohammed Dewji “MO Dewji” ametangaza kuwa  kuanzia October 24 2019 anamtangaza Crescentius Magori  kuwa ndio mshauri wake katika masuala ya soka katika nafasi yake ya uenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Simba SC.

“Napenda kutangaza rasmi kuwa nimemteua Ndg. Crescentius Magori kuwa mshauri wangu binafsi kama Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba. Anauzoefu mkubwa wa soka la Afrika na ninaamini uwepo wake utaongeza nguvu kwenye safari yetu ya kuifanya Simba kuwa moja ya klabu yenye mafanikio makubwa zaidi barani Afrika”>>> MO Dewji

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Crescentius Magori  aliwahi kuwa CEO wa Simba SC kwa kipindi cha miezi sita kabla ya nafasi yake kurithiwa na Senzo Masingiza aliyewahi kuwa CEO wa Orlando Pirates ya Afrika Kusini, Magori pia anahusishwa na kwenda kuwa CEO wa bodi ya Ligi.

VIDEO:CEO WA SIMBA , ALIPOULIZWA HATMA YA AUSSEMS KWAKUTOFIKIA TARGET

Soma na hizi

Tupia Comments