February 14 kila mwaka ni siku ya wapendanao ambayo maarufu sana kwa jina la Valentine’s Day, imezoeleka watu mbalimbali wakiwemo mastaa wakiitumia siku hii kuonesha mapenzi yao kwa wapenzi wao kwa kuwaletea zawadi, kutoka nao kwa ajili ya dinner na mambo mengi.
Kwa upande wa Mwanasoka wa Togo Emmanuel Adebayor ambaye anacheza soka la kulipwa Uturuki, kwa sasa yupo mchini Uturuki na mpenzi wake Dilish Methew raia wa Namibia na ameitumia siku hii muhimu ya Valentine’s Day kwa kumnunulia mpenzi wake maua rose (Red Rose) na kumpatia zawadi.
Wawili hao ambao awali hawakutarajiwa kufika mbali kutokana na majina yao kuwa makubwa, penzi lao linaonekana kuzidi kushamiri tofauti na wengi walivyokuwa wakidhani hawapo serious, Dilish Methew alianza kupata umaarufu mkubwa Afrika baada ya ushindi wake wa Big Brother Africa The Chase 2014, aliamua kuonesha zawadi yake hiyo mtandaoni huku akiambatanisha na maneno “Siku zote amekuwa akifanya kila kitu maalum kheri ya siku ya wapendanao”
“VALENTINE’S HAIWAHUSU WASIO OA AU KUOLEWA, ALIKUFA MTU” MTAALAM