Michezo

Man United pigo juu ya pigo kuelekea game dhidi ya Liverpool

on

Wakati huu club ya Man United ikiwa inaaminika kuwa katika hali mbaya kutokana na kuyumba toka aondoke kocha wao wa zamani aliyekuwa na mafanikio ziaidi Alex Ferguson, sasa inaelekea kucheza mchezo wa Liverpool ikiwa na presha ya kuwa nafasi ya 12 katika msimamo wa Ligi Kuu ya nchini England.

Ikiwa inaelekea kucheza mchezo dhidi ya Liverpool club ya Man United imetoa taarifa mbaya kuhusiana golikipa wao namba moja David De Gea na kiungo wao Paul Pogba ambao imethibitka kuwa ni majeruhi, kufuatia taarifa hiyo sasa ni wazi watawakosa katika mchezo dhidi ya Liverpool Oktoba 20 2019.

De Gea alilazimika kutolewa nje ya uwanja katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Euro 2020 kati ya taifa lake la Hispania dhidi ya Sweden katika sare ya 1-1, hivyo hofu inakuwa kubwa kwani kuumia kwa De Gea kutamfanya Sergio Romero kuingia goli akiwa wengi hawana imani nae kutokana na kukaa benchi na hii ndio itakuwa mechi yake ya kwanza ya Ligi, hivyo De Gea sasa anaungana na Pogba na Jesse Lingard ambao ni majeruhi.

AUDIO: SERGIO AGUERO WA MAN CITY AMEPATA AJALI

Soma na hizi

Tupia Comments