Mix

Wakurugenzi walioteuliwa watakiwa kufika na vyeti siku ya kiapo Ikulu

on

Taarifa niliyoipokwea kutokea ikulu jijini Dar es salaam kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi kuwa ametoa taarifa kwa wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya walioteuliwa kuwa watakapofika Ikulu Dar es salaam kwa ajili ya kula kiapo cha uadilifu wa uongozi wa umma siku ya Jumanne July 12 2016 wahakikishe wanakuja na nakala zao halisi za vyeti vya kitaaluma (Original Academic Certificates).

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uhakiki wa vyeti halisi vya kitaaluma (Original Academic Certificates) unafanywa kwa lengo la kujiridhisha baada ya mchakato wa kawaida wa uhakiki kufanywa kwa kutumia vyeti visivyokuwa halisi (Photocopies).

ULIKOSA HII YA RAIS MAGUFULI ALIVYOMUITA ALIYEPAZA SAUTI’WATANZANIA TUKO NYUMA YAKO’? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments