Mix

Masahihisho ya orodha ya wakurugenzi walioteuliwa na Rais Magufuli leo

on

Taarifa niliyoipokea kutokea Ikulu jijini Dar es salaam imedai kwamba kuna marekebisho madogo katika majina yaliyopo kwenye orodha ya wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya iliyotolewa hapo awali ambapo Dkt. Leonard Moses Massale ametangazwa kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma.

Jina hilo limeingizwa katika Orodha ya Wakurugenzi wa halmashauri kwa makosa na kwa sababu hiyo Dkt. Leonard Moses Massale anaendelea kuwa Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza. Kufuatia marekebisho hayo, uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma utatangazwa baadaye.

ULIKOSA HII YA RAIS MAGUFULI KUELEZA SABABU YA KUSIMAMISHA AJIRA MPYA KWA MUDA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments