Mix

Mapendekezo 9 JPM ameyapitisha kutoka Kamati ya mchanga wa madini

on

Leo May 24, Ikulu Dar es salaam Rais Magufuli amepokea ripoti ya Kamati Maalum iliyoteuliwa na Rais kuchunguza mchanga wa madini kwenye makontena 277 yaliyozuiwa na serikali kusafirishwa kwenda nje kwaajili ya uchenjuaji.

Kamati hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wake Prof. Mruma imemkabidhi ripoti iliyoonesha kuna upotevu mkubwa wa mapato na rasilimali za nchi, ambapo ripoti imesema Tanzania inapoteza kiasi cha Tsh. Bilioni 829.4 hadi Trilioni 1.439 kwa kusafirisha mchanga nje ya nchi.

Prof. Mruma ametoa mapendekezo ya kamati hiyo kuwa kama ifuatavyo.

  1. Serikali isitishe usafirishaji wa mchanga mpaka mrabaha stahiki utakapolipwa kwa kuzingatia thamani halisi ya makinikia.
  2. Tepe za udhibiti zifungwe mara moja ili kuepuka udanganyifu unaoweza kufanyika wakati wa kuchukua sampuli.
  3. TMAA ipime metali zote zilizomo kwenye makenikia ili kupata thamani halisi ya metali hizo( mrahaba).
  4. Kutokana na uwepo wa madini kwenye mbale, TMAA ipime viwango vya metali zote muhimu ktk mbale bila kujali nyaraka za msafirishaji.
  5. Serikali iwachukulie hatua watendaji wa TMAA na wale wa wizara husika.
  6. Pamoja na vyombo vya uhakiki, Serikali iweke mfumo wa kushtukiza ili kuepuka watendaji kufanya kazi kwa mazoea.
  7. Serikali itumie wataalamu wa mionzi ili kufunga scanner zenye uwezo sahihi kwa ajili ya makinikia na mizigo mingine.
  8. Ujenzi wa vinu vya uchakataji ufanyike haraka ili madini yote yaweze kufahamika na kutozwa mrabaha sahihi..
  9. Uchunguzi zaidi ufanywe na wataalam wa mionzi kwenye scanner zinazotumika bandarini ili kubaini aina au mfumo sahihi wa scanner unaofaa.

VIDEO: Rais Magufuli amemtaka Waziri Prof. Muhongo ajiuzulu. Bonyeza hapa chini kuangalia pamoja na mengine ya ripoti ya Kamati ya mchanga wa madini

Soma na hizi

Tupia Comments