Mix

Uteuzi mwingine wa Rais Magufuli leo September 9 2016

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo September  09 2016 amemteua Ado Steven Mapunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara. Ado Steven Mapunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Benedict Richard Ole Kuyan ambaye amestaafu.

Aidha Rais Magufuli amemteua Tixon Tuliangine Nzunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa. Tixon Tuliangine Nzunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Symthies Emmanuel Pangisa ambaye amestaafu. Tarehe ya kuapishwa kwa Makatibu Tawala wa Mikoa walioteuliwa itatangazwa baadaye.

ULIKOSA HII YA RAIS MAGUFULI KUSEMA WANALALAMIKA PESA ZIMEPOTEA…..HII MSG IENDE CLEAR KWAO? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments