Mix

Maamuzi ya Mahakama Ilala kwa Jamaa waliotapeli maduka ya dawa na kujifanya madaktari

on

December 2014 Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ‘NHIF’ ulifungua kesi katika mahakama ya Wilaya Ilala dhidi ya aliyekuwa  mfanyakazi wa hospitali ya IMTU, Bakari Ramadhani na mwenzake Ahmed Mohamed.

May 23 2016 Hakimu wa Mahakama ya Ilala, Hassan Juma ameitoa hukumu kwa watu hao ambapo wamehukumiwa kwenda jela baada ya kukutwa na hatia ya makosa tisa likiwemo la kughushi nyaraka za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ‘NHIF’ na kutapeli maduka makubwa ya dawa mjini hivyo kuisababishia NHIF hasara ya milioni 10.

Mshitakiwa Bakari amekutwa na hatia kwa makosa yote tisa, makosa nane amehukumiwa miaka mitatu kwa kila kosa na miezi 12 kwa kosa la tisa na mshitakiwa Ahmed aliyekuwa anajifanya Daktari amekutwa na hatia ya makosa manne na kwa kila kosa amehukumiwa miaka mitatu. 


ULIKOSA YA ALIYEMTUKANA RAIS MAGUFULI KUFIKISHWA MAHAKAMANI ARUSHA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments