Michezo

Ronaldo kuondoka Juventus?,Man City na Man United watuma ofa

on

Cristiano Ronaldo mapema leo ameripotiwa kwenda katika mazoezi ya Juventus kuagana na wachezaji wenzake wakati huu akihusishwa kujiunga na Man City au Man United.

Mwandishi mahiri wa habari za usajili nchini Italia Fabrizio Romano ameweka wazi kuwa Man City wamejitoa katika mbio hizo za kuwania saini ya Ronaldo na sasa Man United ndio wanapewa nafasi zaidi.

Pamoja na hayo Ronaldo mchana huu ameonekana Airport Turin Italia akipanda ndege binafsi akiwa kaongozana na mpenzi wake Georgina Rodriguez inadaiwa kuwa wanaelekea England.

MESSI AFICHUA PSG WALIVYOMPIGIA SIMU “HUZUNI DAKIKA ZA MWISHO IMESHINDIKA”

TAZAMA MASHABIKI WA BARCELONA WALIVYOISIMAMISHA GARI LA MESSI, SHANGWE ZAIBUKA UFARANSA “PSG”

 

Soma na hizi

Tupia Comments