Top Stories

India maambukizi ya Covid-19 yafikia Milioni 25

on

Maambukizi Nchini India yamefikia Milioni 25, ikiwa ni Taifa la pili ulimwenguni kufikia idadi hiyo baada ya Marekani. Visa vipya 263,533 vimerekodiwa katika saa 24 zilizopita na kupelekea jumla ya maambukizi kuwa Milioni 25.23.

Idadi ya maambukizi mapya imekuwa ikipungua katika Taifa hilo ambalo Hospitali zimekuwa zikilazimika kukataa wagonjwa. Tangu Aprili 21, visa visivyopungua 300,000 vimekuwa vikirekodiwa.

Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya, jumla ya waliofariki dunia imefikia 278,719 baada ya vifo 4,329 kurekodiwa ndani ya siku moja.

RAIS SAMIA ASHONEWA SARE YA KIJESHI “NI NZURI MNOO, NITAIVAA”

Soma na hizi

Tupia Comments