Maajabu

Kwenye zile kali za mwaka !!! hii ya Wanaume 400 kukata uume wao uliipata?

on

Saint_Gurmeet_Ram_Rahim_Singh_Ji_InsanIshu ya imani ni ya mtu binafsi na kila mtu ana uwezo wa kuamini kile anachoona ni sahihi kwa mtazamo wake na mtu anapotokea kumuamini kiongozi wake wa dini kwa asilimia kubwa hutekeleza yale anayofundishwa.

Sasa hii ya leo inamuhusu mhubiri  maarufu wa dini India ambaye ana wafuasi zaidi ya milioni hamsini duniani  Gurmeet Ram Rahim Singh anakabiliwa na mashtaka ya kusababisha majeruhi kwa tuhuma za kuwashawishi wafuasi wake 400  kukata sehemu zao za siri ili waweze kuwa karibu na Mungu.

MSG-The-Messenger-of-God-Movie-Critics-Reviews-Public-Reviews-Ft.-Gurmeet-Ram-Rahim-SinghWafuasi wa Singh walikata sehemu zao za siri kwenye Hospitali ambayo yeye anaimiliki ambapo kwenye headlines nyingine mhubiri huyu amekuwa akihusishwa na mauaji ya mwandishi wa habari za uchunguzi pamoja na kutuhumiwa kwa unyanyasaji wa kijinsia lakini hajawahi kushtakiwa.

Mmoja wa wafuasi wake, Hans Raj Chauhan aliwaambia Polisi kwamba alikatwa sehemu zake za siri kwa sababu alidhani asingetakiwa kwenye jamii kama angekataa kutekeleza utaratibu huo uioanzishwa Singh.

Singh aliwaambia wafuasi wake kwamba wale ambao wanaotekeleza amri hiyo watakuwa na uwezo wa kumuona Mungu.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments