Oktoba mwaka jana chuo kikuu cha Zimbabwe kilipitisha sheria kupiga marufuku wanafunzi wa kike na wa kiume kutopigana mabusu katika mazingira ya chuo, kingine kilichozuiwa ni kukumbatiana na pia ishu ya wanafunzi wa kike au wa kiume kuingia kwenye Hostel za wanafunzi wengine wa jinsia tofauti na zao.
Safari hii kuna taarifa ambayo imeingia kwenye headlines India baada ya kupitishwa Sheria iliyowekwa na moja ya kijiji katika jimbo la Kusini Magharibi ya kupiga marufuku kupigana mabusu hadharani na tabia nyingine ambazo ni kinyume na maadili.
Uongozi wa kijiji hicho cha Salvador -de Mundo kilichopo Kaskazini mwa mji wa Panaji jimbo la Goa, imepitisha sheria hiyo huku ikiwaonya watu wanaotembelea eneo hilo dhidi ya vitendo kama hivyo.
Mmoja wa viongozi wa kijiji hicho Reena Fernandes alisema wameidhinisha sheria hiyo kutokana na malalamiko kutoka kwa wakazi kuhusu wapenzi wanaopigana busu hadharani.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>>twitter Insta Facebook