Maajabu

Hii inahusu punda kushirikishwa kufanya mauaji ya binadamu kutokana na imani za kishirikina.

on

FarasiTumezoea kuona matukio ya kikatili yanayofanyika kutokana na imani za kishirikina hasa pale  mtu anapohisiwa kuwa na matendo ya kishirikina na kufanyiwa matendo ya kinyama kwa wananchi kujichukuli sheria mkononi kinyume cha sheria huku wakijua ni kosa, hii imekuwa tofauti kabisa nchini India.

Polisi inawashikilia watu thelathini wakihusishwa na tukio hilo la kumdhalilisha mwanamke mmoja magharibi mwa India baada ya kumpa adhabu ya kuburuzwa na Punda akiwa nusu utupu, adhabu iliyoamriwa na baraza la kijiji cha Panchayat.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka arobaini na tano alifanyiwa kitendo hicho baada ya kushutumiwa kumuua binamu yake kwa imani za kishirikina.

Familia ya mwanamke huyo iliuchoma mwili wake na kuuzika kabla ya kutoa taarifa kwa polisi.
Kama utapenda kutopitwa na kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments