Michezo

Infantino adaiwa kupambana kumng’oa Ahmad Ahmad CAF

on

Rais wa Club ya Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini Patrice Motsepe anatajwa kuwa Rais Mpya wa CAF baada ya Ahmad Ahmad kuelekea uchaguzi Mkuu wa CAF March 12 2021 nchini Morocco.

Inaripotiwa na Waandishi mbalimbali Afrika kuwa Rais wa FIFA Gianni Infantino amewashauri Jacques Anouma, Augustin Senghor na Ahmed Yahya kujitoa na kumuunga Mkono Motsepe ili amshinde Ahmad Ahmad.

Inaripotiwa kuwa Rais wa FIFA Infantino na Rais wa sasa wa CAF Ahmad Ahmad haziivi tena na sasa, Infantino anatumia nguvu nyingi kuhakikisha Ahmad Ahmad harudi tena madarakani baada ya jaribio la kumfungia kugonga mwamba kwa Mahakama ya Kimichezo Duniani (CAS) kutengua uamuzi wa FIFA.

Soma na hizi

Tupia Comments