Rapper Kanye West ‘Ye’ ameamua kujivua gamba kwenye masuala ya siasa na kutaka kujikita zaidi kwenye masuala yake binafsi hii ni baada ya kudai kuwa watu hawaoni umuhimu wake pamoja na kumpa sapoti Rais Donald Trump.
Kupitia ukurasa wa twitter wa Kanye West ameandika “Macho yangu yamefunguka vya kutosha na sasa nimetambua kuwa nimekuwa nikitumika kusambaza jumbe ambazo hata mimi mwenyewe siziamini. Ninakaa mbali na siasa na kujikita zaidi kuwa mbunifu”
Inadaiwa kuwa ujumbe huo aliouandika Kanye West kupitia ukurasa wake wa twitter ni baada ya kushambuliwa na mashabiki kutokana na wengi kuonekana kutopenda sapoti aliyokuwa akimpa Rais Donald Trump huku ikiwa inaelezwa kuwa Rais Trump ni mbaguzi wa rangi.
Kanye West amekanusha ishu inayomuandama hivi karibuni kuwa anahusika na utengenezaji wa T-shirts zenye logo ya ‘BLEXIT’ ujumbe ambao umetafsiriwa kushawishi watu weusi wakikimbie chama cha Democratic.
Vituko vya ‘PAPA MAFIDOO’ shuleni, begi la nguo abebea daftari