Top Stories

Injinia huyu asukumiwa “Waziri utapata BP ukiona banda, limejengwa kwa Milioni 100” (+video)

on

Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa ameamuru kukamatwa msimamizi wa mradi Mhandisi Alistides Kanyomo(50) wa kampuni ya Mbesso Contruction Ltd ya Dar es Salaam inayomilikiwa na Fidelis Bachwa kwa kushindwa kutekeleza mradi kwa wakati pia kutoridhishwa na gharama za ujenzi wa mradi huo unaogharimu shilingi Bilioni sita.

Aidha Mbarawa ameshangazwa gharama za ujenzi wa ofisi ya muda ambayo imejengwa kwa shilingi million mia moja, Profesa Mbarawa ametilia shaka kutokuwepo kwa ubao wa mradi (Sign board) ambao umetozwa gharama ya shilingi milioni kumi ambao hata hivyo haukuwepo eneo la ujenzi wa mradi.

Hata hivyo Mbarawa amesitisha mkataba wa mkandarasi huyo na kuagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi wa haraka ili kubaini uhalisia wa bei za mradi huo.

MFUNGWA AGOMA KURUDI NYUMBANI KISA MKEWE “NILIMKATA NA SHOKA”

Soma na hizi

Tupia Comments