Ad

Michezo

Hii ndio Top 10 ya wachezaji soka maarufu katika mtandao wa Instagram duniani …

on

Mtandao wa kijamii wa Instagram umeanzishwa miaka mitano iliyopita ila toka kuanzishwa kwake unatajwa kuwa miongoni mwa mitandao ya kijamii inayokuwa kwa kasi zaidi duniani, huu ndio mtandao ambao maarufu kwa watu kupost picha na video zao. December 10 mtu wangu naomba nikusogezee Top 10 ya mastaa maarufu zaidi katika mtandao wa Instagram yaani wanafollowers wengi.

Cristiano Ronaldo ambaye ni mkali wa kuvunja rekodi za soka kwa sasa ndio staa wa soka anayetajwa kuwa na wafuasi wengi katika mitandao yote ya kijamii. Huenda ukawa unashangazwa na list ya wachezaji wa America kuwa wengi katika list hii, ukweli ni kwamba America mtandao wa Instagram unatajwa kuwa na watumiaji milioni 400 na milioni 39.5 kati ya hao wamewafollow wachezaji soka wakubwa. Hii ndio Top 10 mtu wangu.

10- Thiago Silva wa klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa (PSG) ana followers milioni 8

62838

Thiago Silva

9- Karim Benzema wa klabu ya Real Madrid ya Hispania na timu ya taifa ya Ufaransa ana followers milioni  8.3

Benzema6-1024x1024

Karim Benzema

8-Ronaldinho ambaye aliwahi kuchezea timu ya taifa ya Brazil ila kwa sasa hana timu ana jumla ya followers milioni 8.7 .

Dinho-1024x1024

Ronaldinho

7- Zlatan Ibrahimovic mshambuliaji wa klabu ya PSG ya Ufaransa na timu ya taifa ya Sweden ana followers milioni 10.

zLATAN

Zlatan Ibrahimovic

6- David Luiz listi hii wachezaji wa Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa wametawala, yeye ana followers milioni 11.

dAVID

David Luiz

5- Gareth Bale ni mchezaji anayeshikilia rekodi ya usajili ya Dunia anaitumikia klabu ya Real Madrid ya Hispania na timu ya taifa ya Wales ana jumla ya followers milioni 11.4

Bale11

Gareth Bale

4- James Rodriguez anakipiga katika klabu ya Real Madrid anatajwa kufikia followers milioni 16.7

R2-1024x999

James Rodriguez

3- Lionel Messi wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina anatajwa kuwa na followers milioni 30.5

Messi-g

Lionel Messi

2- Neymar ndio mchezaji wa pili wa FC Barcelona kuwa katika hii list ana followers milioni 36.5

Neymar-vg

Neymar

1- Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ndio anatajwa kuwa staa maarufu zaidi katika mitandao ya kijamii ikiwemo instagram ana followers milioni  39.4

Ronaldo34-1024x1024

Cristiano Ronaldo

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments