Baada ya sakata la video chafu la msanii wa Bongo Fleva na video vixev maarufu kama Amber Rutty kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, RC Paul Makonda amemtaka msanii huyo kujisalimisha kituo cha polisi kilichopo karibu yake kabla saa kumi na mbili jioni.
RC Paul Makonda ametumia ukurasa wake wa instagram kutoa tamko hilo na kusisitiza kuwa endapo Amber Rutty atafika kituo cha polisi atakuta ujumbe wake tayari kutoka kwa polisi.
“Wakati TCRA wakijipanga kuchukua hatua, mimi namtaka mwenye picha hii kufika kituo chochote Cha Polisi kilichopo karibu na eneo lake kabla ya 12 jioni. Na ukifika waambie umeitwa na Rc Makonda watakupatia ujumbe wako”
MO KUTEKWA | Suti yenye Bullet Proof | Kumvalisha JK, Sheria Ngowi aongelea yote