Forbes imemtaja rapper mkongwe Snopp Dogg kuwekeza kwenye moja ya Benki kubwa na yenye utajiri mkubwa nchini Sweden.
Forbes wametoa ripoti na kusema kuwa Rapper huyo amewekeza kwenye Benki ya Klarna ambayo inatajwa kuwa ni Benki ya mtandaoni inayotoa huduma za kununua bidhaa papo hapo na malipo hufanyika baadae kupitia mawakala wao zaidi ya 100,000 barani Ulaya na Marekani.
Snoop Dogg ametajwa kuwa kinara wa kampeni mpya ya Kampuni hiyo ‘SMOOTH’ imemfanya Snoop kubadilisha jina na kutaka kujiita ‘Smooth Dogg’. Benki hiyo inatajwa kufikia utajiri wa zaidi ya Shilingi Trilioni 6 za Kitanzania ambapo Snoop amewekeza hisa za watu wachache ambazo ni hisa zisizozidi asilimia 50.
ULIPITWA NA TAARIFA ZA ALIKIBA KUFIWA NA BABA YAKE /MTU WA KARIBU KATHIBITISHA /CHANZO CHA KIFO?