Top Stories

UPDATE: Mahakama yamwachia huru mfanyabiashara Shamba Mollel

on

Mahakama ya Hakimu Mkazi  Arusha imemuachia huru mfanyabiashara maarufu jijini Arusha Methiew Shamba Mollel baada ya kumkutana hana hatia katika kesi ya kughushi muhtasari wa mtaa wa Levolosi ili kupata hati miliki ya kumiliki shamba.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Gwatwa Mwankuga amesema amepitia vyema ushahidi wa walalamikaji wapatao kumi na kujiridhisha kuwa hakuna kesi ya msingi ya kujibu katika malalamiko hayo na kwamba mlalamikaji aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisutu Dan  Makanga hajairidhisha mahakama juu ya malalamiko dhidi ya mshtakiwa.

Ulipitwa na hii? VITUKO HAVIISHI: Wakili Feki kaingia kazini Mahakama Kuu bila wasiwasi

Wamiliki IPTL/ESCROW wamefikishwa tena Kisutu leo, Maamuzi ya Mahakama je?

Soma na hizi

Tupia Comments