Mix

Kwa watumiaji wa simu za Iphones na Android hii inawahusu

on

 

Mtandao wa WikiLeaks umetoa ripoti kuhusu CIA ku-hack watumiaji wa simu za Iphones na Androids jana  March 7 2017 , katika ripoti hiyo wamesema CIA wamekuwa  wakiingilia mazungumzo binafsi ya watu wa kawaida wasiokuwa na madhara kwa taifa ambapo wamekua wakiona message binafsi kama WhatsApp.

CIA pia wame-hack simu zinazoingia na kutoka tangu mwaka 2013  hadi 2016, picha na kila kitu mtu anachofanya kwenye simu yake ya Androids na Iphones,  ripoti hiyo pia imeishutumu CIA ku-hack TV aina ya Samsung kwa kuweka kifaa kinacho rekodi mazungumzo binafsi hata kama TV ikiwa imezimwa.

Wamiliki wa kampuni za Iphones  na Androids wanaendelea kuchunguza taarifa hiyo iliyoogopesha watumiaji wa simu  za aina hiyo, kwani taarifa ya kichunguzi inasemekana CIA  wanafuatilia pasipo makampuni ya utengenezaji wa simu hizo kujua.

ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV MARCH 8 2017? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI.

Soma na hizi

Tupia Comments