Iran imetekeleza mashambulizi makubwa dhidi ya Israel kwa kutumia makombora ya balistiki zaidi ya 200 huku ikidaiwa kuwa makombora mengi yamenaswa, haswa katika anga ya Jerusalem na Tel Aviv.
Jeshi la Israeli limezungumzia juu ya kuongezeka kwa uhasama “mbaya na hatari”, hali ambayo itakuwa na athari kubwa. Tehran inasema iko tayari kupiga “miundombinu yote ya Israeli” ikiwa serikali ya Kiyahudi italipiza kisasi.
Iran inasema shambulio hilo la makombora ni la kulipiza kisasi mauaji ya mwezi Julai ya kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh, pamoja na kiongozi wa Hezbollah, Hassan Nasrallah, siku ya Ijumaa – na kwa mauaji ya watu wa Lebanon na Wapalestina.
Lakini majeraha madogo mawili yaliripotiwa.
Televisheni ya taifa ya Iran imeangazia taarifa kutoka kwa IRGC (lslamic Revolution Guard Corps) ikithibitisha kuwa “makumi” ya makombora yamerushwa kuelekea Israel, na kutishia shambulio jingine iwapo Israel itajibu.
Wizara ya mambo ya nje ya Iran imelitaka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lichukue hatua za maana kuepusha vitisho dhidi ya amani na usalama wa Mashariki ya Kati.